Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa misaada kwa wakimbizi wa ndani Libya

IOM yatoa misaada kwa wakimbizi wa ndani Libya

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM kwa kushirikiana na asasi za kiraia 37 limeanza kugawa misaada isiyo ya chakula kwa raia walipoteza makazi katika makambi sehemu mbalimbali nchini Libya hususan katika mji wa Tripoli.

Kwa mujibu wa msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe msaada huo unailenga jamii ya Tawerika yenye watu takriban 30,000 ambao walilazimika kuhama makadi yao wakati wa machafuko nchini humo.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)