Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO kusaidia radio za kijamii Uganda

UNESCO kusaidia radio za kijamii Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni, UNESCO, litatia shime juhudi za vyombo vya habari vya kijamii nchiniUgandakatika kutimiza wajibu wa vyombo hivyo kwa maendeleoa ya jamii nchini humo.UNESCO itadhamini uzinduzi rasmi wa Mtandao wa radio za kijamii nchini Uganda  COMNETU tukio litakalowaleta pamoja wadau wa vyombo hivyo ikiwemo Tume ya mawasiliano, Chama cha waandishi wa habari wanawake, UMWA, na radio mbalimbali za kijamii.

Uzinduzi huo unatarajiwa kuwa chachu ya kukuza lengo kuu la radio za kijamii la kusaidia maendeleo kwa kutoa elimu, taarifa na burudani ili kuleta mabadiliko mazuri.

Uzinduzi huo unaofanyika mwishoni mwa wiki hii jijiniKampala ni mwendelezo wa mjadala wa kitaifa kuhusu maendeleo kupitia mawasiliano ulioendeshwa na chuo kikuu cha Makerere kupitia kitengo chake cha uandishi na mawasiliano.