Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu ya mafua ya H7N9 bado yaighubika China:WHO

Hofu ya mafua ya H7N9 bado yaighubika China:WHO

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO  hadi sasa visa 24 vya mafua aina ya H7N9  vimebainika katika majimbo manne nchiniChinahuku watu 7 wakipoteza maisha kutokana na maradhi hayo. WHO inasema hakuna maambukizi baina ya binadamu kwenda kwa binadamu lakini mwenendo unafuatiliwa kwa karibu. Shirika la chakula na kilimo FAO na wizara ya kilimo yaChinawanashirikiana kutafuta chanzo cha mafua hayo, kwani nguruwe sio chanzo na sasa wanafuatia kwa karibu soko la kuku.Msemaji wa WHO ni Gregory Hartl.

(SAUTI YA GREGORY HARTL)