Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awa na mazungumzo na Pope Francis huko Vatican

Ban awa na mazungumzo na Pope Francis huko Vatican

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekuwa na mazungumzo na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pole Francis wa kwanza huko Vatican, Italia ambapo amesema kiongozi huyo ana wamejadili jinsi ya kufanikisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia kwa kuhakikisha usimamizi wa haki miongoni mwa jamii. Bwana Ban amesema ilikuwa ni heshima kubwa kuwa na mazungumzo na Pope Francis wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa umezindua rasmi kipindi cha Siku Elfu moja kuelekea ukomo wa malengo ya milenia. Waandishi wa habari walimuuliza Katibu Mkuu juu ya taarifa za kuongezeka kwa mvutano katika rasi yaKoreana hofu ya jaribio la nyuklia kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea kulikosababisha kufungwa kwa eneo la viwanda laKaesong.

 (SAUTI YA BAN)

 “Mamlaka za Pyongyang zinapaswa kuangalia kile kinachoendelea duniani zama hizi za utandawazi. Na serikali hiyo inapaswa kujitahidi zaidi kuboresha ustawi na matumaini ya wananchi wake badala ya kuongeza hofu na mvutano, badala ya kuchukua mwelekeo hasi na wa kichochezi.”

Bwana Ban amesema tayari amekuwa na mazungumzo na viongozi waChinakuhusu sualahilona pia alhamisi atajadili na Rais Barack Obama wa Marekani. Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Ban amekuwa na mazungumzo na viongozi wa serikali ya Italia ambako wamejadili pia masuala ya mizozo hukoSyria,Malina Ukanda waSahelna jinsi ya kupatia suluhisho la kudumu mizozo hiyo.