Kuelekea siku ya afya duniani, mfumo wa maisha wachochea magonjwa

3 Aprili 2013

Takiwmu za shirika la afya duniani WHO zinaonyesha kwamba Kila mtu mzima mmoja kati ya watatu duniani ana ongezeko la shinikizo la damu, hali ambayo inasababisha karibu nusu ya vifo vyote vitokanavyo na kiharusi, na maradhi ya moyo.

Takwimu hizi ni kutokana na ripoti mpya ya shirika la afya duniani ambayo pia inasema mtu mzima mmoja kati ya kumi duniani ana ugonjwa wa kisukari.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Margaret Chan anasema  katika mataifa ya kipato cha juu, upimaji na tiba ya gharama nafuu imesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa matatizo ya shinikizo la damu na hivyo kupunguza idadi ya vifo.

Hata hivyo nchi za Afrika zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Tanzania ikiwa moja wapo zaidi ya asilimia 40 hadi 50 ya watu wazima wanakadiriwa kuwa na shinikizo la damu.

George Njogopa amefanya mahojiano na Dk Simon Shita jijini Dar es salaam, ncini Tanzania  anayeelezea namna ya kuepuka magonjwa hayo yasiyo yakuambikizwa ikiwemo shinikizo la damu tunapoelekea siku ya afya duniani April 7, ambayo inaangazia ugonjwa huo.