Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa ombi la dola miloni 70 zaidi kwa oparesheni zake eneo la maziwa makuu

UNHCR yatoa ombi la dola miloni 70 zaidi kwa oparesheni zake eneo la maziwa makuu

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linatoa ombi la dola milioni 70 zaidi kwa oparesheni zake mwaka 2013 kuwasaidia maelefu ya raia waliolazimika kuhama makwao katika eneo la maziwa makuu.

Fedha hizo ni kwa wale waliohama makwao kutokana na mzozo ulioshuhudiwa kwenye mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na kwa wakimbizi wa ndani wanaorejea makwao. Fedha hizo zinajumuisha dola milioni 22 kwa DRC, dola milioni saba kwa taifa la Burundi, dola milioni 17 kwa Rwanda na dola milioni 22 kwa taifa la Uganda.

Fedha hizi ni juu ya dola milioni 282 za bajeti ya mwaka 2013 zilizoidhinishwa mwaka uliopita na bazara kuu la UNHCR kufadhili oparesheni zake kwenye nchi hizo nne. Msemaji wa UNHCR, Adrian Edwards, anaeleza fedha hizi zitatumika kwa mahitaji gani

SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

 “Pesa hizo ni muhimu katika kugharamia mahitaji muhimu kwa takriban raia 450 wa DRC waliohama makwao ndani mwa DRC na nje mwa mipaka yake kutokana na ghasia za mwaka uliopita mkoni Kivu kaskazini na Kusini wakiwemo wakimbizi 5,600 nchini Burundi, 23,000 nchini Rwanda na 35,000 nchini Uganda. Ombi hilo pia litagharamia mahitaji ya watu 50,000 waliohama makwao na wengine 50,000 wanaotarajiwa kurudi makwao mwaka huu wakiwemo wakimbizi 5400 nchini Burundi, 11,000 nchini Rwanda na 40,000 nchini Uganda.”