UNRWA yalaani mauaji ya watoto wa Kipalestina nchini Syria

UNRWA yalaani mauaji ya watoto wa Kipalestina nchini Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowasaidia Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limelaaani shambulizi lililofanywa nchini Syria likiwalenga watoto wa Kipalestina ambao ni wanafunzi katika shule mbalimabli.

Kwa mujibu wa Shirika hilo mashambulizi hayo mfululizo yaliyowalenga wakimbizi wa Kpalestina waishio Syria yamesababisha vifo vya watu wanne akiwamo  mototo mwenye umri wa miaka 14 aliyepata jeraha kichwani huku wengine wakijeruhiwa.

UNRWA imesema katika taarifa yake ya kwamba vitendo endelevu vya mashambulizi kwa Wafungwa Wakipalestina na jamii za Wasiria  vinasikitisha na kuongeza kwamba wafanyaji wa ghasia hizo wanapaswa kulaaniwa kwa kuwa wanahatarisha usalama na haki za watoto na raia wasio na hatia.

Shirika hilo limekwenda mbali zaidi kwa kusema hakuna jeshi au maslahi yoyote ya  kisiasa yanayoweza kuhalalisha mauaji kama hayo na kusisitiza mgogoro wa Syria kumalizwa kwa njia ya majadilaino na makubaliano na sio kwa mapigano.