Ban alaani majaribio ya zana za nyuklia nchini Korea Kaskazini

12 Februari 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelaani hatua ya Korea Kaskani ya kufanya majaribio ya zana za kinyumlia hii leo .Ban amesema kuwa hatua hiyo ni ukiukaji mkubwa wa mkataba wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Ban mara kwa mara amekuwa akitoa wito kwa utawala mpya wa taifa la Korea Kaskazini wa kutaka kufanyika kwa mabadiliko na kuboresha uhusiano wake na jamii ya kimataifa.

Katibu mkuu ameelezea wasi wasi wake kutokana na athari na msukosuko utakaosababishwa na hatua hii katika eneo hilo akiitaka Korea Kaskazini kufanya mikakati ya kuangamiza zana za kinyuklia. Ban anasema kuwa ana uhakika kuwa baraza la usalama la Umoja litachukua hatua zinazohitakjika akiongeza kuwa atafanya mashaurino na pande zote na kuzisaidia kwenye jitihada zao.