Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yaitaka Libya imkabidhi aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi kwake

ICC yaitaka Libya imkabidhi aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi kwake

Majaji wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, imeamuru kuwa serikali ya Libya imkabidhi aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi katika serikali ya Muammar Gaddafi, Abdullah al-Senussi kwa mahakama hiyo mara moja.

Serikali ya Libya bado inamshikilia pia mwanae Gaddafi, Seif al-Islam, na imekuwa ikisisitiza kwamba inapanga yenyewe kumshtaki na kumhukumu Bwana Senussi.

Mapema wakati wa vita vya mapinduzi ambavyo hatimaye vilimtimua Gaddafi mamlakani, mahakama ya ICC ilitoa waranti ya kumkamata Bwana Senussi, kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji na ukatili dhidi ya waandamanaji.