Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio ya Umoja wa Mataifa enzi hizo

Radio ya Umoja wa Mataifa enzi hizo

Jumatano ya tarehe 13 mwezi huu wa February, mamilioni ya watu duniani kote wanasherehekea siku ya Radio duniani. Tukio hili linalenga kuonyesha nguvu ya radio na umuhimu wa matangazo yake yanayofikia mamilioni ya watu kwa nia ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha.

Maadhimisho haya yanarejelea mwaka 1946 ambapo Umoja wa Mataifa uliamua kuanzisha radio yake yenyewe. Na katika basi makala haya maalum ya siku ya Radio duniani Joshua Mmali anamulika miaka ya mwanzoni kabisa ya Radio ya Umoja wa Mataifa.