Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP na wadau kujadili uchafuzi wa mazingira Ongoniland

UNEP na wadau kujadili uchafuzi wa mazingira Ongoniland

Wawakilishi wa Shirika la Mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP, wakiongozwa na Mwakilishi maalum, Erik Solheim, watakutana na viongozi wa ngazi ya juu nchini Nigeria na wadau wengine wiki hii mijini Abuja na Port Harcourt kujadili jinsi ya kutekeleza mapendekezo ya ripoti ya uchunguzi wa UNEP kuhusu uhifadhi wa mazingira katika Ongoniland.

Ripoti hiyo ilochapishwa Agosti mwaka 2011, ilionyesha kuwa uchafuzi wa mazingira katika Ongoniland kwenye jimbo la Niger Delta ulikuwa umeenea tangu miaka ya 1950, na unaathiri vibaya mno mazingira.

Utekelezaji wa hatua za dharura kurekebisha hali hiyo na kuondoa madhara kwa jamii za eneo hilo unatarajiwa kugharimu dola bilioni moja mwanzoni.