Bunge la Urusi litupilie mbali muswada wa propaganda za ushoga.

1 Februari 2013

Kundi la wataalamu huru wa masuala ya haki za kibinadamu la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa bunge la Urusi kutupilia mswada  ambao utaidhinisha kutolewa kwa adabu kwa propaganda zozote zinazohusu ushoga kwa watoto.

Wataalamu hao wanaonya kuwa mswada huo utakandamiza haki za binadamu nchini Urusi na kuwalenga zaidi walio mashoga , wasagaji na wale wanaobadili jinsia zao ambao tayari wamelegwa pakubwa nchini humo.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetesi wa haki za binadamu Margaret Sakaggya ameonya kuwa sheria hiyo itatumika kukandamiza shughuli za wale wanaotetea haki za mashoga , wasagaji na wale wanaobadili jinsia zao. Wataalamu hao wanasema kuwa bado kuna fursa ya  kubadilisha mswada huo wakati itakaposomwa bungeni akiwataka wabunge kuutupilia mbali mswada huo ili kuhakikisha kuwepo kwa haki za binadamu nchini Urusi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud