Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la UM laahidi kuwaunga mkono wananchi wa Haiti

Baraza la Usalama la UM laahidi kuwaunga mkono wananchi wa Haiti

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamewahakikishia wananchi wa Haiti kwamba jamii ya kimataifa imejitolea kuunga mkono jitihada zao za kutafuta amani , uthabiti pamoja na maendeleo.

Hii ni kupitia taarifa iliyotolewa na Rais wa baraza hilo Masood Khan inayojiri baada ya kupokea ripoti kutoka kwa mwakilishi mkuu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa ujumbe wa wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH Mariano Fernandez kuhusu hali nchini Haiti.

Wajumbe wa baraza hilo wanasema kuwa wanatambua hatua zilizopigwa kwenye nyanja za usalama ambazo zimekuwa zikiungwa mkono na MINUSTAH.

Wameezishauri pande zote za kisiasa nchini Haiti kuongeza juhudi zao katika kudumisha uthabiti na usalama uliopatikana kwa muda wa mwaka mmoja uliopita.

Pia waliunga mkono umuhimu wa kuandaliwa kwa uchaguzi ulio huru na wa haki ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kwa minajili wa kuhakikisha kuwepo kwa mazingira yaliyo muhimu kweye ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.