Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabunge wa nchi za makuu wajadili amani kwenye ukanda wao

Wabunge wa nchi za makuu wajadili amani kwenye ukanda wao

Mkutano wa tatu wa wabunge wa nchi za maziwa makuu umeanza leo huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC ambapo washiriki kutoka nchi 12 za maziwa makuu wanataka kuwepo kwa amani ya kudumu kwenye maeneo ya migogoro ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mashariki mwa DRC, na baina ya Sudan na Sudan Kusini.

Katibu mtendaji wa mkutano wa kimataifa kwa nchi za Maziwa Makuu, Ntumba Luaba amesema washiriki wahakikishe wanatia shime kwa dhati na kupitisha maazimio ambayo yatawezesha vikundi visivyotakia mema ukanda wa maziwa makuu kutokomezwa ifikapo mwaka 2014 ili kutoa fursa kwa harakati za kutokomeza umaskini.

Rais wa zamani wa Burundi, Sylvestre Ntibantunganya ambaye kwa sasa ni seneta ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo na amesema suluhisho la mgogoro kwenye Maziwa Makuu linapasa kuzingatia katiba ya kila nchi.

(SAUTI YA NTIBANTUNGANYA)