Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe maalum wa UM kuhusu ubaguzi wa rangi azuru Uhispania

Mjumbe maalum wa UM kuhusu ubaguzi wa rangi azuru Uhispania

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi Mutuma Ruteere ameanza ziara ya juma moja nchini Uhispania ambapo anatarajiwa kukutana na waakilishi wa serikali , wabunge , mahakama, Ombudsman, mashirika yasiyokuwa ya serikali pamoja na makundi yanayofanya kazi kwneye nyanja za ubaguzi wa tangi. Ruteere tayari ashakutana na Waziri wa masuala ya kigeni Gonzalo Benito.