Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wanaorejea Niger wapatiwa stadi

Wahamiaji wanaorejea Niger wapatiwa stadi

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limezindua mpango wa kuwasaidia wahamiaji raia wa Niger wanaorejea nyumbani kutoka Libya pamoja na familia zinazowahifadhi.

Mradi huo ambao tayari umepokea Euro milioni 2.8 kutoka kwa jumuiya ya Ulaya utasaidia kubuni miradi itakayochangia mapato kwa watu 3,125 moja kwa moja kutoka sehemu za Tahoua, Tillabery, Zinder na mji mkuu Niamey.

IOM inasema kuwa wale wanaorejea nyumbani watapata mafunzo ya siku tatu jinsi wanavyoweza kupata mapato yakiwemo ya kusimamia biashara ndogo ndogo, kilimo cha mboga na matunda, useremara na ufugaji.