Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unyanyapaa bado wakwamisha udhibiti wa Ukimwi

Unyanyapaa bado wakwamisha udhibiti wa Ukimwi

Shirika lisilo la kiserikali linahusika na HIV na Ukimwi nchini India limetaja changamoto zinazolikabiili katika kazi ya kusaidia waathirika wa ugonjwa huo ikiwemo uhaba wa fedha na unyanyapaa.

Loon Gange, ambaye ni Rais na mwanachama mwanzilishi wa DNP+ amesema kuwa ameshuhudia watu wengi wakiaga dunia kwa sababu hawakutibiwa kutokana na uhaba wa fedha na wengine kuona haya kujitokeza kutokana na unyanyapaa.

Shirika hilo "The Delhi Network of Positive People" (DNP+) lilanzishwa mwaka 2000 na watu wawili likiwa na lengo la kusaidia na kuhakikishia maelfu ya watu wanapata tiba na kwamba hata sasa wanagombana na changamoto za utetezi kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimw na Ukimwi..

Kutoka mwanzo wake wa hali ya chini DNP+ imekuwa na kufikisha wanachama 1300 na mwaka jana ilipata ilipewa tuzo ya Red Ribbon kwa kazi yake ya kibinadamu.