Mwegemeo wa imani za kidini wadhihirika katika mapigano nchini Syria: Tume huru

20 Disemba 2012

Mgogoro unaoendelea nchini Syria umeripotiwa kuchukua mwelekeo wa kidini ambapo baadhi ya vikundi vinalazimika kupambana ili kujilinda au kuonyesha mshikamano na moja ya pande zinazozozana katika mgogoro huo.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Tume huru iliyoundwa kuchunguza mzozo wa Syria ambapo imesema majeshi ya serikali na wanamgambo wenye silaha wamekuwa wakishambulia raia wa madhehebu ya Sunni.

Kwa upande wao wapinzani wa serikali wanashambulia waalawite na jamii nyingine ndogo zinazounga mkono serikali kama vile wakatoliki, waarmeniani, waothodoksi na wadruze.

Tume hiyo imesema raia wanaendelea kukumbwa na madhara yatokanayo na mzozo huo wakati huu ambapo mapigano yamejikita hadi maeneo ya mijini. Kwa mantiki hiyo kufanyika kwa mashauriano ya kisiasa ili kumaliza mgogoro huo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud