Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yapata kiongozi mpya: Ni Mohamed Ibn Chambas

UNAMID yapata kiongozi mpya: Ni Mohamed Ibn Chambas

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wamemtangaza Mohamed Ibn Chambas kuwa kiongozi mpya wa UNAMID ambao ni ujumbe wa pamoja wa pande mbili hizo wa kulinda amani kwenye jimbo la magharibi mwa Sudan, Darfur.

Bwana Chambas ambaye ni raia wa Ghana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ibrahim Gambari ambaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Nkhosazana Dlamini-Zuma wamesifu huduma aliyotoa wakati wa utendaji wake.

Majukumu ya Mkuu wa UNAMID iliyoundwa mwaka 2007 ni pamoja na kuwa msuluhishi mkuu wa mgogoro huko Darfur akiwakilisha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.