Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uandikwaji wa rasimu kuhusu mageuzi ya mawasiliano wakamilika: UM

Uandikwaji wa rasimu kuhusu mageuzi ya mawasiliano wakamilika: UM

Wajumbe zaidi ya 160 waliokuwa wanakutana huko Doha, wamekamilisha hatua ya kwanza muhimu ya uandikaji wa rasimu ambayo inakusudia kutumika kwa ajili ya kuyafanyia marekebisho miongozo ya mawasiliano duniani.

Kukamilika kwa rasimu hiyo kutafanikisha mageuzi ya sheria ambayo sasa itaruhusu uhuru wa kusafirisha taarifa duniani kote bila vikwazo vyovyote.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mawasiliano ITU, limesema kuwa wajumbe hao wamafaulu kuandika awamu ya kwanza ya rasimu hiyo ambayo inatazamiwa kujadiliwa siku za usoni.