Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto waliathirika kiakili katika mapigano ya Gaza: UNICEF

Watoto waliathirika kiakili katika mapigano ya Gaza: UNICEF

Uchunguzi wa awali uliofanywa kuhusu athari za kiakili kufuatia siku nane za mapigano ya Gaza mapema mwezi Novemba umeonyesha kuwa watoto waliathirika sana kisaikolojia. Zaidi ya watoto mia tano walihojiwa katika uchunguzi huo uliofanyika kati ya Novemba 24 na 25.

Zaidi ya asilimia 90 ya watoto chini ya miaka 12 walisema kuwa wanaogopa milio au sauti za juu, na wanakumbwa na jinamizi wanapolala. Takriban idadi kama hiyo ya vijana walobalehe wameelezea pia kuathiriwa kwa njia kama hiyo.

UNICEF inasema imeweka bajeti ya dola milioni 3 kwa ajili ya ulinzi wa watoto na kuwapa ushauri nasaa. Ili kufanya hivyo, UNICEF imetambua familia 21 ambazo zitatoa nafasi salama kwa wanawake na watoto kwenda kupokea misaada ya kuwasaidia kukabiliana na hali hii. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)