Mabadiliko ya hali ya hewa yaendelea huku ulimwengi ukitazama: WMO

28 Novemba 2012

Kuyeyuka kwa haraka kwa barafu eneo la kaskazini mwa dunia na hali mbaya ya hewa vyote vinavyoshuhudiwa kote duniani ni ishara tosha kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanaendelea huku ulimwengu ukitazama.

Hii ni kwa mujibu Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kwenye taafira yake ya hivi punde kuhusu hali ya hewa duniani. WMO inasema kuwa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani kunaendelea, na miezi ya kwanza ya mwaka 2012 imeingia kwenye kumbukumbu kama kipindi cha joto la juu zaidi tangu kumbu kumbu hizo zianze kuwekwa mwaka 1850.

Karibu kilomita milioni 12 mraba za barafu zimeyeyuka na kuingia baharini kati ya mwezi March na Septemba mwaka huu n kulingana na WHO hii ni dalili kuwa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa yanaendelea. Michel Jarraud ni mkuu wa WMO.