Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya kutoa misaada yarejelea shughuli za utoaji misaada Goma: UNHCR

Mashirika ya kutoa misaada yarejelea shughuli za utoaji misaada Goma: UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na washirika wake wamerejelea shughuli zao za kuwasaidia wakimbizi wa ndani kwenye maeneo 12 mjini Goma kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambapo misaada inatolewa ikiwemo chakula, sabuni na vyombo vya maji.

Usambazaji wa misaada ulianza mwishoni mwa wiki ukiwalenga watu 110,000. Hi ndiyo shughuli ya kwanza kubwa ya utoaji misaada kufanywa tangu mji wa Goma ulipotekwa na waasi wa M23 Novemba 20. Wengi wa waliohama wanasema wana nia ya kurudi makawao huku utoaji misaada zaidi ukipangwa kwenye maeneo watakayorejea. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

Wakimbizi wengi wa ndani wanahitaji makao na maji safi. Usafi umesalia kuwa changamoto kutokana na kutokuwepo kwa choo na vituo vya maji. Visa vya kutapika na kuendesha vimeripotiwa tayari. Matatatizo haya ya kupumua yanatokana na sababu kuwa watu hawana makao na wanalala nje kwenye mvua.