Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya ulanguzi wa watu ni wajibu wa kila mmoja:Ezeilo

Vita dhidi ya ulanguzi wa watu ni wajibu wa kila mmoja:Ezeilo

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Joy Ngozi Ezeilo amezitaka biashara kote duniani kuacha kutumia wafanyikazi wanaosafirishwa kiharamu na pia kuchunguza na kuzuia wafanyikazi kama hao wanaotumia wa washirika wao.

Bi Ezeilo amesema kuwa katika ulimwengu wa sasa ulanguzi wa binadamu unapatikana kwenye sekta zote zikiwemo za kiuchumi na unaathiri mataifa yote yakiwemo wanakotoka , wanakoptia na vituo vyao vya mwisho.

Bi Ezeilo ameyasema haya wakati wa kukamilika kwa mkutano wa wataalamu wa kimataifa mjini Ankara nchini Uturuki ambapo zaidi ya watalamu 20 kuhusu ulanguzi wa watu walikusanyika wakiwemo pia wataalamu kutoka nyanja za kibiashara, haki za binadamu, kutoka kwa mshirika ya kimataifa na waakilishi kutoka mashirika makubwa duniani. Jason Nyakundi na taarifa kamili.