Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji kuwa msingi mkuu wa maendeleo kwa nchi za Asia na Pacific

Usafirishaji kuwa msingi mkuu wa maendeleo kwa nchi za Asia na Pacific

Wawakilishi kutoka mataifa 23 ya Asia na Pacific leo wameanza mkutano wao wa siku tatu huko Bangkok, Thailand unaojadili ushirikiano katika ujenzi wa mtandao bora na wa uhakika wa barabara baina ya nchi hizo ambao utachochea ukuaji wa uchumi huku ukitoa fursa kwa wananchi wote kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii.

Mkutano huo umeandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya uchumi na kijamii kwa nchi za Asia na Pacific, ESCAP na unatathmini mpango wa kikanda uliopitishwa mwaka jana kuhusu mtandao wa usafirishaji kwenye eneo hilo.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa ESCAP Dkt. Noeleen Heyzer ameieleza kamati ya usafirishaji ya Tume hiyo kuwa sekta ya usafirishaji ina nafasi kubwa katika kupunguza umaskini, kuchochea ukuaji wa uchmi na kuleta maendeleo.

(SAUTI YA DR. NOELEEN HEYZER)