Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zimbabwe yapigwa jeki kupambana na Ukimwi

Zimbabwe yapigwa jeki kupambana na Ukimwi

Zimbabwe iko katika mwelekeo mzuri kufikia utimilifu wa utoaji huduma za matibabu kwa wagonjwa wa virusi vya UKIMWI pamoja na wale wanaougua kifua kikuu.

Hatua hiyo inafuatia msaada wa fedha kutoka fuko la kimataifa la Global Fund iliyotoasi kiasi cha doka za kimarekani milioni 84.

Pamoja na mambo mengine fedha hizo zinatazamia kufanikisha mpango wa usambazaji wa madawa ya kufubaza ukali wa virusi vya HIV ARVs.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana zaidi ya wagonjwa 480,000 wanatazamiwa kufaidika na mpango wa usambazaji wa dawa hizo.