Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Afrika wazungumzia migogoro kwenye Baraza Kuu la UM

Viongozi wa Afrika wazungumzia migogoro kwenye Baraza Kuu la UM

Viongozi wa Afrika wanaohudhuria mkutano wa kilele wa baraza la Umoja wa Mataifa mjini New York wameanza kutoa hutuba zao huku wakilenga zaidi maeneo yanayohusu mikwamo ya vita na kuzorota kwa huduma za kibanadamu.

Viongozi hao wamesema kuwa maeneo hayo kwa kiasi kikubwa yanasalia kuwa kikwazo kinachorudisha nyuma nchi za afrika kusonga mbele kimaendeleo

Akihutubia kikao hicho cha 67, rais wa Benin Boni Yayi aliitolea mwito jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi za kuwafurusha wanamgambo wa kiislamu ambao wamelizingira na kuliteka eneo la kaskazini mwa Mali.

Rais huyo amesema kuwa kuendelea kuwepo kwa kundi hilo la waasi kuhatarisha usalama wa eneo nzima la Afrika Magharini hivyo ametoa mwito kwa jumuiya ya kimaifa kuziunga mkono juhudi zinazoendeshwa sasa zenye shabaha ya kuwafurusha wanamgambo hao.

Wanamgambo hao wa kundi la Tuareg wametwaa eneo la Kaskazini mwa Mali na wameanzisha shabaha ya kusambaza sheria ya kidini sharia huku wakiazimia kuyateka maeneo mengine zaidi.

Wito kama huo umetolewa pia na marais wengine kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Liberia na Senegal.