Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afanya majadiliano na rais wa Iran kuhusu mzozo wa Syria na hali ya mashariki ya kati

Ban afanya majadiliano na rais wa Iran kuhusu mzozo wa Syria na hali ya mashariki ya kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekuwa na mazungumzo na rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad ambaye yuko New York kuhudhuria mkutano wa kila mwaka unaowaleta pamoja wakuu wa nchi ulimwenguni kote ambao wanachama wa Umoja huo wa Mataifa.

Viongozi hao wamejadilia hali ya mambo nchini Syria na huko Mashariki ya Kati. Ban amwelezea mwenezake namna anavyoingia na huzuni kufuatia mapigano yanayoendelea kuchacha nchini Syria ambayo yamezorotesha ustawi wa kijamii.

Katika mada nyingine, Ban ameitaka Iran kutafuta suluhu ya kimataifa juu ya mpango wake wa kuendelea na vinu vya kinuklia na amesema taifa hilo linapaswa kujijengea uaminifu mbele ya sura ta kimataifa kuhusiana na mpango huo wa kinyuklia

Kadhalika Ban amekutana na viongozi wa mataifa mengine na ikiwemo Waziri Mkuu wa Kuwait Mubarak Al Hamad Al Sabah,Waziri wa Mashauri ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle na marais kadhaa akiwamo wa Bulgaria Rosen Plevneliev.