Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahitaji ya kibinadam yaongezeka wakati idadi kubwa ya Wasyria wakitoroka makwao:WFP

Mahitaji ya kibinadam yaongezeka wakati idadi kubwa ya Wasyria wakitoroka makwao:WFP

Mahitaji ya kibinadam, hasa yale ya chakula, yanaendelea kuongezeka, huku idadi kubwa ya raia wa Syria wakitoroka makwao, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. Ripoti hiyo pia inasema kuwa hali ya usalama inaendelea kuzorota katika vitongoji vya mji mkuu Damascus, huku hali ya taharuki ikiwa imetanda mjini Aleppo, na watu wengi wakitafuta makazi katika majengo ya umma kama vile misikiti, shule na makanisa.

Shirika la WFP limesema kuwa linaongeza shughuli zake za utoaji misaada ili kuwafikia watu milioni 1.5 na msaada wa chakula katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Shirika hilo pia limesema wengi wa watu waliotoroka makwao wamelazimika kuhama mara mbili, kama vile waliotoroka mji wa Homs na kukimbilia Aleppo. Muhannad Hadi ni mkurugenzi wa WFP nchini Syria.

(SAUTI YA MUHANNAD HADI)