Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kuwasafirisha wahamiaji 275 wa Ethiopia waliokwama Yemen

IOM kuwasafirisha wahamiaji 275 wa Ethiopia waliokwama Yemen

Wahamiaji 275 kutoka Ethiopia, na ambao wamekwama nchini Yemen, watarejeshwa mjini Addis Ababa mnamo Jumanne Septemba 25 kwa ndege, chini ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM. Safari hiyo ambayo imefadhiliwa na msaada wa dola milioni 2.1 kutoka kwa serikali ya Uholanzi, itakuwa ya tatu ya aina yake, baada ya safari mbili kama hizo kufanyika Jumanne na Jumatano wiki hii, na ambazo ziliwachukua wahamiaji 551.

Wahamiaji hawa wanaorejeshwa wanawakilisha asilimia 25 ya wajamiaji wote karibu 4,000 kutoka Ethiopia, ambao hawana makazi na wanaishi kwenye maeneo ya wazi katika mji wa Haradh, kaskazini magharibi mwa Yemen.

Wahamiaji wote walikuwa wamejaribu kuvuka mpaka na kuingia Saudi Arabia kutafuta ajira, lakini wakashindwa na hivyo kukwama Yemen. Kwa sababu za uhaba wa fedha, IOM inalazimika kuwapa kipaumbele wale ambao wanakabiliwa na hatari zaidi, wakiwemo wanawake, watoto na watu wazee. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)