Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani Ban atoa wito kwa ulimwengu kusitisha uhasama

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani Ban atoa wito kwa ulimwengu kusitisha uhasama

Ni waimbaji wa Umoja wa Mataifa, wakiimba wimbo wa amani, kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani, katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii ya amani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa ulimwengu mzima kusitisha uhasama. Bwana Ban amemsihi kila mmoja kote ulimwenguni kutafakari kwa dakika moja, kuhusu wale waliofariki kutokana na mizozo, wale walionusurika lakini bado wanaishi na uchungu , na wale ambao wanateseka sasa hivi na kukumbwa na ukiukaji mkubwa wa haki zao.

Kauli mbiu ya siku ya leo ni amani endelevu kwa ajili ya siku zijazo endelevu, na Bwana Ban amesema mizozo hushambulia misingi ya maendeleo endelevu

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Vita vya silaha hushambulia misingi ya maendeleo endelevu. Mali ya asili inatakiwa kutumiwa kwa manufaa ya jamii, sio kufadhili vita. Watoto wanatakiwa kuwa shuleni, sio kuajiriwa kama wanajeshi. Bajeti za kitaifa zinastahili kuangazia mahitaji ya watu, na sio silaha kali.

(BELL- 5 secs, and fade under)

Hafla hiyo ambapo imepigwa kengele ya amani mjini New York imehudhuriwa na mabalozi, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, pamoja na mabalozi wema wa amani, wakiwemo nyota wa filamu Forest Whitaker na Michael Douglas.