Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya nyuklia inaweza kutumika katika uzalishaji wa Kilimo

Teknolojia ya nyuklia inaweza kutumika katika uzalishaji wa Kilimo

Shirika la Kimataifa la IAEA limeandaa kongamano la kujadili matumizi ya nguvu za nyuklia katika uzalishaji wa kilimo.

Kongamano hili limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zinazokubali mwelekeo wa IAEA, wa kutumia teknolojia ya sayansi ya nyuklia kwa njia ya amani.

Ili kufahamu zaidi, Joshua Mmali kutoka Idhaa ya redio ya UM amezungumza na Profesa Miriam Kinyua, ambaye ni mhadhiri wa Bayoteknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya, anayehusika na utafiti katika mimea ya ngano na mihogo, na ambaye amealikwa kwenye kongamano hilo ili kuzungumzia jinsi teknolojia ya nyuklia inavyoweza kutumika kwa uzalishaji wa chakula cha kutosha kwa siku zijazo.

(MAHOJIANO YA JOSHUA NA PROF. MIRIAM)