Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay akaribisha ripoti ya ghasia za mwaka 2010 nchini Thailand

Pillay akaribisha ripoti ya ghasia za mwaka 2010 nchini Thailand

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi pillay amekaribisha kutolewa kwa ripoti ya mwisho ya tume ya haki na maridhiniano nchini Thailand kuhusu ghasia za mwaka kisiasa za mwaka 2010 akiitaja hatua hiyo kama mwelekeo wa kuwepo uwajibikaji na maridhiano nchini Thailand. Maandamano ya kati ya mwezi Aprili na May mwaka 2010 yaliyotokea nchini Thailand yalisababisha ghasia ambapo watu 92 waliuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa.

Pillay amesema kuwa hata kama kumekuwepo na vizingiti tume hiyo imefanya uchunguzi ulio muhimu kuhusu ghasia za kisiasa na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Thailand. Alice Kariuki  na taarifa kamili.

(SAUTI YA  ALICE KARIUKI)