Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usikilizaji rufaa ya Khmer Rouge wakamilika Cambodia

Usikilizaji rufaa ya Khmer Rouge wakamilika Cambodia

Mahakakama ya uhalifu wa kivita nchini Cambodia ambayo inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa imekamilisha kusikiliza rufani ya watuhumiwa wa uhalifu uliofanywa wakati wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo Khmer Rouge.

Uhalifu huo uliotendeka wakati wa utawala wake miongo mitatu iliyopita. Kiongozi huyo alikutikana na hatia ya  kuendesha mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.

Wakati wakiwasilisha utetezi wao, marafiki zake kiongozi huyo walirejelea kudai kuwa hakuwa na mafungamano yoyote na utawala wa Khmer Rouge, na wala hawakuhusika kwenye njama zozote za kihalifu. Hata hivyo wamedai kuwa kwa nyakati fulani walilazimika kutekeleza agizo toka mamlaka za juu na kama wangepuuzia basi wangeuwawa.