Ligi ya mabingwa wa kandanda barani Asia yajiunga kwenye kampeni ya kukabiliana na njaa

17 Septemba 2012

Kampeni ya kupiga vita njaa ya ligi ya kandanda barani Asia inaanza tena wiki hii, wakati wa kuanza mechi za raundi ya mchujo mnamo Jumatano tarehe 19. Wakati wa mechi hizo zitakazoendelea hadi Novemba, mashabiki wa kandanda watatakiwa kuungana ili kuongeza misaada kwa watu wanaokabiliwa na tatizo la njaa.

Kufuatia ufanisi wa kampeni ya mwaka ulopita ambapo zaidi ya dola 400, 000 zilichangishwa na Shirikisho la Soka Barani Asia (AFC) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO) ili kuzisaidia familia maskini vijijini na jamii zingine barani Asia, mashirika hayo mawili yanaungana tena na vilabu vya ligi ya mabingwa barani Asia ili kuchangisha pesa kwa ajili ya miradi ya pamoja ya FAO na AFC barani Asia.George njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)