Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alitaka bunge la Uswis kuendelea kuzisaidia nchi masikini

Ban alitaka bunge la Uswis kuendelea kuzisaidia nchi masikini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza Jumanne kwenye bunge la Uswis amesema analitaka bunge hilo kuendelea kujikita katika ksaidia nchi masikini na wanaohitaji msaada.

Ban ameongeza kuwa ni muhimu bunge hilo likashirikiana na Umoja wa mataifa ili kuhakikisha kwamba mipango ya kukabiliana na mdororo wa kiuchumi haiathiri vita vya dunia dhidi ya uumasikini. Amelitaka pia bunge hilo kusaidia juhdi za Umoja wa Mataiofa za kuhakikisha malengo ya maendeleo ya milenia yanafikiwa ambayo muda wake wa mwisho uliowekwa ni mwaka 2015 na unakaribia.

Masuala mengine ambayo Katibu mkuu ameyagusia akihitaji msaada wa Uswis ni muongozo wa majadiliano ya mabadiliko ya hali ya hewa, kkabiliana na tishio la nyuklia na hasa kuondoa mkwano katika mkutano wa upokonyaji wa silaha.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)