Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka ghasia zikomeshwe Darfur baada ya vifo

UM wataka ghasia zikomeshwe Darfur baada ya vifo

Mkuu wa mpango wa amani wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Darfur, UNAMID ametoa wito yakomeshwe mapigano katika mji wa Kutum kaskazini mwa jimbo la Darfur, ambayo tayari yameshababishwa vifo kadhaa.

Amesema amesikitishwa kuwa watu wa mji wa Kutum wamekabiliwa tena na uchungu na mateso, na kutaka uhasama wote ukomeshwe mara moja. Katika taarifa yake, kaimu mwakilishi maalum wa UNAMID, Aichatou Mindaoudou ametoa wito kwa wahusika wote kushiriki mazungumzo ya amani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vikosi vya kulinda amani vya UNAMID karibu na mji wa Kutum, ulioko takriban kilomita 100 kutoka mji mkuu wa Darfur wa El Fasher, vimeripoti kuwa hali ya usalama ilianza kuzorota mnamo siku ya Jumanne, tarehe 4 Septemba, pale ulipotokea ufyatuaji risasi na jaribio la kumwua kiongozi mmoja wa mikoa. George Njogopa na taarifa kamili

(TAARIFA YA GEORGE)