Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani uharibifu katika eneo la kidini la Sufi nchini Libya

UM walaani uharibifu katika eneo la kidini la Sufi nchini Libya

Wataalamu watatu huru wa Umoja wa Mataifa wamelaani uharibifu wa maeneo ya kidini na ya kihistoria ya Sufi kwenye sehemu mbalimbali za Libya na pia vitendo vya vitisho na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi waandamanaji wasio na silaha wanaopinga uharibifu huo.

Wamesema serikali inapaswa kuchukua hatua dhidi ya uharibifu huo la sivyo utaendelea na kusambaa kwingineko. Wataalamu hao wamesema vitendo hivyo ni ukiukaji wa haki za binadamu hasa haki ya uhuru wa kidini na imani ikiwemo haki ya kulindwa kwa waumini wa dini za walio wachache na maeneo yao ya kuabudu, pia haki ya kufurahia na kupata fursa ya urithi wa kitamaduni.Wameitaka serikali ya Libya kuchukua hatua zote muhimu kulinda maeneo ya kitamaduni nay a kidini ambayo yako hatarini.

(Jason Nyakundi anaripoti)

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)