Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi waliokimbia Libya kwenda Tunisia sasa kupewa makazi Ujerumani:IOM/UNHCR

Wakimbizi waliokimbia Libya kwenda Tunisia sasa kupewa makazi Ujerumani:IOM/UNHCR

Baada ya miezi 18 ya kusubiri katika kambi ya muda iliyopo kilometa saba kutoka mpaka wa Libya na Tunisia sasa wakimbizi 195 wataondoka Jumatatu ijayo kwenda kuanza maisha mapya nchini Ujerumani.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameandaa ndege itakayowasafirisha kutoka Djerba kuelekea Frankfurt kwa niaba ya serikali ya Ujerumani baada ya kusafirishwa kwa basi toka kambi ya muda ya Shousha hadi uwanja wa ndege wa Djerba.

 IOM pia imewafanyia vipimo vya afya wakimbizi hao kabla ya kuondoka. Ingawa Ujerumani imekubali kuchukua wakimbizi 200 watano wakiwemo mama wawili wajawazito wataahirisha safari kwa sababu za kiafya. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)