Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ni lazima zishirikiane katika mitazamo kuhusu sekta ya Posta:UM

Serikali ni lazima zishirikiane katika mitazamo kuhusu sekta ya Posta:UM

Wiki chache kabla ya kufunguliwa kongamano la kimataifa kuhusu hatma ya huduma za posta, Mkurugenzi wa mashirika maalum katika Umoja wa Mataifa, Edouard Dayan amesema serikali kote duniani zinapaswa kubadilishana mawazo kuhusu mtazamo zilizo nao kwa ajili ya sekta ya posta, ili kudumisha umuhimu wake kama sehemu muhimu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, pamoja na uwiano wa kijamii.

Kongamano hilo la mawaziri linaloandaliwa na Muungano wa Kimataifa wa Posta, na ambalo ni la 25 la aina yake, litaanza tarehe 8 Oktoba katika mji wa Doha nchini Qatar.

Bwana Dayan amesema kuwa posta ni mtandao mathubuti, unaoufikia umma, na serikali ni lazima ziangalie ni jinsi gani zinaweza kuutumia katika kuitikia baadhi ya masuala ambayo yanaukabili umma kwa sasa.