Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasyria wanaokimbilia Jordan watasababisha wimbi kubwa la wakimbizi:UNHCR

Wasyria wanaokimbilia Jordan watasababisha wimbi kubwa la wakimbizi:UNHCR

Kiwango cha watu wanaowasili kutoka kwenye mpaka wa Syria na kuingia kwenye kambi ya Za’atri Kaskazini mwa Jordan kimeongezeka mara mbili wiki iliyopita limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Wati zaidi ya 22,000 wamepokelewa katika kambi ya Za’atri tangu ilipofunguliwa Julai 30 mwaka huu.

Wakimbizi hao wanasema wenzao kwa maelfu bado wanasubiri kuvuka mpaka wakati huu ambao mapambano yameshika kasi Syria na eneo zima la Daraa na kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Melisa Fleming wanaamini huu utakuwa mwanzo wa wimbi kubwa kabisa la wakimbizi kuingia Jordan. Ameongeza kuwa kuna ongezeko la haraka la watu wanaotoka Syria na kuingia Uturuki ambako watu takribani 5000 wamekuwa wakiwasili kila siku katika muda wa wiki mbili zilizopita.