Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benomar akaribisha hatua ya Kufanyia Ukarabati Sekta ya Ulinzi Yemen

Benomar akaribisha hatua ya Kufanyia Ukarabati Sekta ya Ulinzi Yemen

Mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen amekaribisha hatua iliyopitishwa na Rais wa Yemen Abed Rabbo Mansour Hadi tarehe 6 Agosti mwaka huu inayohusu kuipanga upya sektan ya ulinzi ya nchi hiyo.

Amesema kupitishwa kwa hatua jizi kunakuwa ni hatua muhimu ya utekelezaji wa maafikiano ya kipindi cha mpito ya November 2011 ya kuanzisha mazingira muhimu na kuchukua hatua zinjazohitajika za kuunganisha jeshi chini ya uongozi uongozi wa kitaifa kwa kuzingatia utawala wa sheria.

Mshauri huyo maalumu bwana Benomar anaunga mkono hatua hizi na amezitolea wito pande zote nchini Yemen kufanya kazi pamoja kuhakikisha utekelezaji wa hatua hizo ambazo ni muhimu sana katika kuchagiza amani na utuluvu nchini Yemen.