Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yapunguza matarajio ya mavuno ya mpunga kwa mwaka 2012

FAO yapunguza matarajio ya mavuno ya mpunga kwa mwaka 2012

Shirika la chakula na kilimo FAO limeshusha matarajio yake ya kimataifa ya zao la mpunga kwa mwaka 2012 kutokana na mvua chache za Monsoon nchini India, lakini limesema kwa jumla mazao ya mpunga duniani bado yatasalia kuwa ya juu kuliko mwaka 2011.

FAO imeshusha maratajio ya mpunga mwaka huu kwa tani milioni 7.8 kutokana na kupungua kwa asilimia 22 kwa mvua za monsoon India katikati ya mwezi Juulai hali ambayo itapunguza mavuno kwa msimu wa mwaka huu.

Matarajio ya mavuno pia yamepunguzwa katika mataifa ya Cambodia, Taiwan, Korea Kaskazioni na Kusini na Nepal kwa mjibu wa toleo la FAO la jarida la Julai mwaka 2012 linalofuatilia soko la mchele mduniani. Hata hivyo toleo hilo la Jumatatu linasema mavuno ya jumla duniani yanatarajiwa kupita kiwango kilichofikiwa mwaka 2011 na kuna imani kwamba tani milioni 724.5 za mpunga zitavunwa.