Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya Kimataifa imetakiwa kufanya juhudi za Kukabiliana na hali nchini Mali

Jamii ya Kimataifa imetakiwa kufanya juhudi za Kukabiliana na hali nchini Mali

Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa Antonia Guterres ametoa wito wa jamii ya kimataifa kufanya kila iwezalo kukabiliana na hali iliyopo nchini Mali na kuzitaka nchi kusadia oparesheni ambazo sasa hivi zinakabiliwa na uhaba wa fedha kwenye eneo hilo ambalo halina uwezo wa kujilisha.

Zaidi ya watu 250,000 wameikimbia Mali kwa muda wa miezi sita iliyopita kulipotokea mapigano kati ya vikosi vya serikali, wanamgambo wa Tuareg na makundi kadha yaliyojihami. Kwa sasa kuna wakimbizi 96,000 kutoka Mali walio nchini Mauritania na 53,000 nchini Niger na wengine nchini Burkina Faso huku watu 174,000 wakiwa ni wakimbizi wa ndani. Akiongea kwenye mkutano wa wanahabari mjini Geneva baada ya kufanya ziara ya siku tatu nchini Burkina Faso bwana Geterres amesema.

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)