Moto Waunguza Soko kwenye Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya

2 Agosti 2012

Moto mkubwa uliochoma soko katika Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya mwishoni mwa wiki umeonyesha haja ya kuwa na maandalizi bora ya moto na usalama Katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani.

Moto ulizuka siku ya Jumapili jioni katika soko la kambi ya Dagahaley ambayo ni moja ya makambi tano katika Kambi kubwa ya Daadab kaskazini mashariki mwa Kenya. Asilimia 80 ya soko iliangamizwa. Baadhi ya makazi jirani yaliharibiwa na mali kuibiwa wakati wakaazi walipokimbia.

Soko hili limekuwa kama mji ndani ya Kambi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita na limekuwa likiuza karibu kila kitu kutoka mboga hadi simu za mkononi. Sasa hizi zote zimechomeka na watu wengi wamepoteza mali zao na njia ya kukidhi maisha. Alice Kariuki na taarifa kamili

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter