Maisha ya Wakimbizi wa Ndani nchini Kenya

27 Julai 2012

Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2002 nchini Kenya taifa hilo la Afrika Mashariki lilitumbukia kwenye machafuko yaliyodumu kwa muda wa miezi mitatu, machafuko yaliyotajwa kuwa mabaya zaidi kuwai kushudiwa tangu uhuru. Machafuko hayo yalijiri baada ya pande kuu mbili zilizokuwa ziking’ang’ania kuunda serikali kukosa kuelewana kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais wakati huo.

Jambo hili liliwalazimu wafuasi wa upinzani kuingia barabarani na mitaani kupinga matokeo ya uchaguzi jambo lililochochea machafuko. Ghasia zilizofuata zilisambaa kwa haraka kwenda sehemu nyingi nchini Kenya na wakati wa kipindi hicho cha miezi mitatu zaidi ya watu 1000 waliuawa na maelfu ya wengine wakakimbia makwao kujitafutia usalama. Wengi walitafuta usalama makanisani, shuleni na sehemu zingine za umma ambazo walipata kuwa salama na hadi sasa baadhi yao wamesalia kwenye sehemu hizo kwa kipindi cha miaka minne unusu sasa. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi amefuatilia maisha ya wakimbizi wa ndani nchini Kenya na kutuandalia makala ifuatayo

(MAKALA NA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud