Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kutembelea Myanmar

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kutembelea Myanmar

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya haki za binadamu nchini Myanmar anatazamiwa kutembelea eneo hilo akiwa na dhima ya kutathmini hali ya mambo.

Tomás Ojea Quintana anatazamiwa kuwa huko kuanzia July 30 hadi August 4 akitathmini hali jumla ya haki za binadamu pamoja na maendeleo mengine.

Taifa hilo linapitia kwenye mageuzi makubwa ikiwemo yale yanayohusu sheria na uimarishaji wa mifumo ya demokrasia. Akizungumzia hali jumla ya taifa hilo, mtaalamu huyo ameonyesha matumaini yake akisema Myanmar imeanza kuangaza vyema