Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uholanzi yatoa dola milioni 2.1 kwa IOM kuwasaida Wahamiaji kutoka Pembe ya Afrika

Uholanzi yatoa dola milioni 2.1 kwa IOM kuwasaida Wahamiaji kutoka Pembe ya Afrika

Shirika  la kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesema kuwa serikali ya Uholanzi imetoa dola milioni 2.1 kusaidia juhudi zake za kuwasaidia wahamiaji kutoka pembeni mwa Afrika, ambao wamekwama nchini Yemen wakijaribu kwenda Saudi Arabia.

Mchango huo ambao ndio mkubwa zaidi kutoka kwa serikali ya Uholanzi kwa harakati za IOM Mashariki ya Kati, utatumiwa kutoa huduma za kibinadamu kwa maelfu ya wahamiaji ambao wamekwama nchini Yemen bila chao, na ambao kwa kawaida hupitia mateso makubwa wakiwa wanajaribu kwenda kutafuta ajira na usalama katika mataifa ya guba.