Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali eneo la Sahel yazidi kuwa mbaya Kutokana na kuripotiwa Mkurupuko wa Kipindupindu

Hali eneo la Sahel yazidi kuwa mbaya Kutokana na kuripotiwa Mkurupuko wa Kipindupindu

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi kutokana na kuripotiwa mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwenye sehemu kadha za eneo la Sahel Magharibi mwa Afrika ambapo maelfu ya watu kwa sasa wameathiriwa na ukame. Kati sehemu zilizoathirika zaidi ni pamoja na Niger, kaskazini mwa Mali ambapo mvua zinazonyesha zimesababisha hali kuwa mbaya zaidi hasa kwenye kambi wanakoishi waliokimbia ghasia nchini Mali.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa maji yaliyo na ugonjwa huo kutoka mto Niger ndicho chanzo cha ugonjwa huo. Nalo shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa tayari watoto wawili wameaga dunia kaskazini mwa mali kutoka na ugonjwa wa kipindupindu huku vifo 56 vikiripotiwa nchini Niger na visa 2,242 vya ugonjwa huo vikiripotiwa tangu mwanzo wa mwaka huu. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)