Hatua za Kimataifa zinahitajika ili Kuzuia Ghasia nchini Syria:Ban

9 Julai 2012

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon amesema kuwa hali nchini Syria inazidi kuwa mbaya akisema ukiukaji wa haki za binadamu unaendelea nchini humo yakiwemo mauaji. Akihutubia waandishi wa habari Ban amesema kuwa kwa sasa Takriban watu milioni 1.5 wanahitaji misaada ya dharura ya kibinadamu.

Kwenye mkutano wake wa kwanza mjini Geneva kundi kuhusu Syria liliafikiana mpango wa mabadiliko utakaofuatwa nchini Syria likiwemo suala la kubuniwa kwa idara itakayohusika na mabadiliko ikiongozwa na wanachama wa serikali ya sasa na upinzani. Kundi hilo pia lilitaka pande zinazozozana kuachana na ghasia na kushirikiania na waanagalizi wa Umoja wa Mataifa walio nchini humo na pia kutekeleaza mpango wa amani wa pande sita uliopendekezwa na Annan.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter